Searching...
Tuesday, July 20, 2010

Mto mrefu zaidi wa China wakumbwa na mafuriko makubwa

Taarifa iliyotolewa tarehe 20 na ofisi ya uongozi wa kazi ya kukabiliana na mafuriko na maafa ya China inasema, kutokana na mvua kubwa kunyesha kwa mfululizo katika siku za karibuni, mto Changjiang ambao ni mto mrefu wa kwanza nchini China umekumbwa na mafuriko makubwa ambayo hayajatokea tangu mwaka 1987.

Saa 2 asubuhi ya tarehe 20 maji yaliyotoka sehemu ya juu ya mtiririko wa mto Changjiang yalifika kwenye bwawa la magenge matatu lililopo sehemu ya katikati ya mto huo. Hii ni mara ya kwanza mradi huo mkubwa kabisa wa maji duniani kukumbwa na mafuriko makubwa tangu ujenzi wake ukamilike mwaka 2008. Habari zinasema ndani ya saa 24 kuanzia saa 2 asubuhi ya tarehe 19 hadi saa 2 asubuhi ya tarehe 20, kiwango cha maji kwenye bwawa hilo kilipanda kwa karibu mita mitatu, na bwawa la magenge matatu limefanikiwa kuzuia maji ya mafuriko yenye mita za ujazo bilioni 1.5.

Serikali ya China imeagiza serikali katika mikoa mbalimbali iliyopo kando ya mto Changjiang iimarishe ukaguzi wa kingo za mto. Hivi sasa watu zaidi ya milioni 1.96 wanafanya kazi ya kukabiliana na mafuriko kando ya mto Changjiang.

Mbali na hayo mto, Huaihe ambao ni mto mwingine mkubwa wa mashariki mwa China pia umekumbwa na mafuriko, na kiwango cha maji kwenye sehemu ya juu ya mtiririko wa mto huo pia kimezidi kile cha tahadhari.

Habari na Idhaa ya china

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!