Idadi ya waliofariki katika ajali ya treni nchini India yapanda na kufikia 61
Idadi ya watu waliofariki kwenye ajali mbaya ya treni nchini India imepanda na kufikia 61. Idadi hiyo ambayo mchana wa leo ilikuwa imetajwa kuwa 48 imepanda baada ya majeruhi kadhaa kufariki wakiwa hospitalini. Zaidi ya watu 50 pia wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo. Afisa mmoja wa serikali ya India amesema ajali hiyo ilitokea baada ya treni ya abiria kugonga treni nyingine iliyokuwa imesimama katika mji wa Sainthia kwenye jimbo la Bengal Magharibi. Duru za shirika la reli la India zinasema kuwa ajali hiyo imesababishwa na kutowajibika kwa makandawala wa magarimoshi hayo.
0 comments:
Post a Comment