Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF inasema usambaaji wa chini kwa chini wa virusi vya HIV Ulaya Mashariki na Asia unaongezeka katika kiwango cha kutisha.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ongezeko la maambukizi linachochewa na matumizi ya mihadarati, ngono sisizo salama na tabia ya unyanyapaa inayowafanya watu wengi wasititafute taarifa za jinsi ya kuzuia au matibabu.
Ripoti hiyo "laumu na fukuza" inaeleza jinsi ukimwi wa chini kwa chini unavyoathiri watoto Ulaya Mashariki na Asia ya Kati, inatanabaisha mambo yanayowakabili watoto wanaoishi na virusi vya HIV, watoto wanaojihusisha na ngono isiyo salama, wanawake wajawazito wanaotumia mihadarati na pia inaeleza kwamba kuna zaidi ya watoto na vijana milioni moja wanaoishi au kufanya kazi mitaani katika maeneo hayo.
0 comments:
Post a Comment