Kwa mujibu wa 'gazeti' la Sun la nchini Uingereza, ile Safina ya Nuhu ambayo Waktristo na wasomaji wa Biblia wameisoma au kusimuliwa inasemekana ipo nchini Uturuki kwenye umbali wa futi 13,000 katika mlima mmoja nchini humo.
Kikundi cha Wainjilisti na Wavumbuzi wa Mambo ya Kale (archeologist) kutoka China na Uturuki wamesema kuwa wameyapata mabaki ya vipande vya mbao katika Mlima Ararat ulioko Mashariki mwa Ururuki.
Wavumbuzi hao wanasemakuwa kipimo cha kung'amua umri wa vitu kwa kitaalam, 'carbon dating' kinathibitisha kuwa mabaki hayo yana umri wa miaka 4,800 - muda ambao unashabihiana na muda unaosomeka katika vitabu vya dini na historia kuwa ndipo safina hiyo ilipoelea juu ya maji.
Mmojawapo wa wachambuzi hao, Dk. Yeung, amekanusha taarifa kuwa inawezekana hayo ni mabaki ya shughuli za kibinadamu wa hivi karibuni kwa kusema kuwa shughuli za kibinadamu hazijathibitika kuwepo katika eneo hilo lenye mwinuko wa futi zipatazo 11, 000.
0 comments:
Post a Comment