Miss Chumbageni kufanyika Aprili 30
MASHINDANO ya kuwania taji la Miss Chumbageni mkoani Tanga, litafanyika Ijumaa ya Aprili 30, kwenye Ukumbi wa Club la Tanzanite. Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kampuni ya Apple Partners Group waandaaji wa shindano hilo na kutiwa saini na Mratibu wake, Susan Ihunga ilisema kuwa awali shindano hilo lilikuwa lifanyike Mei Mosi, lakini sasa litafanyika Aprili 30.
"Unajua Mei Mosi kuna pilikapilika nyingi za Sikukuu ya Wafanyakazi, sasa tunataka watu washiriki kikamilifu sherehe hizo na sisi tunataka kuwapata raha siku moja kabla," alisema Ihunga.
Alisema maandalizi kwa ajili ya mashindano hayo yameiva na kuwa sehemu kubwa ni kuibua warembo wenye vipaji kwa ajili ya mashindano la
Miss Tanga na baadaye Miss Tanzania.
Ihunga alisema kuwa warembo wote wamekwishaanza mazoezi tayari kwa mashindano hayo yanayotarajiwa kuwa ya aina yake mkoani Tanga kwa kuwa yanafungua pazia la mashindano ya urembo
ngazi ya vitongoji.
Alisema baada ya mashindano hayo, warembo watatu wataingia kwenye mashindano ya Miss Tanga baadaye Juni na washindi watatu wa shindano hilo la Miss Tanga watakwenda kwenye mashindano ya
Kanda ya Kaskazini.
Mpaka sasa, taji la Miss Tanzania linashikiliwa na Miriam Gerald wa Mwanza aliyelitwaa Oktoba 2, mwaka jana, kwenye Ukumbi wa mliman City
0 comments:
Post a Comment