Searching...
Monday, April 26, 2010

JANA NILIPATA FURSA YA KUTEMBELEA NGOME KONGWE YA GOLCONDA ILIYOPO HAPA HYDERABAD

Hii ni moja ya sehemu za kivutio cha utalii nchini india,ngome hii ni kubwa sana ni kilima kirefu uwezi kuimaliza labda siku nzima.hapa ni mwanzo kabisa wakati unaelekea juu kwenye kilele cha ngome.
nikiwa njiani kuelekea kwenye kilele cha ngome niliona si vibaya kupata kumbukumbu kidogo.
jamani ni kilima kirefu nipo na mdau wangu na pia ni m/kiti wa jumuiya ya wanafunzi wanaoishi hapa Hyderabad,tupo hoi tukaamua kupumzika kidogo ngome ni refu sana kama mbovu uwezi panda.
Hapa kama inavyoonekana kwa juu kabisa hila bado hatujafika kwenye kilele cha ngome
mdau akaona naye si vibaya kupata kumbukumbu tukiwa ndo tunakaribia kufika kileleni mwa ngome
Nami sikuwa nyuma nikaona ni vyema nichukue kidogo kumbukumbu hapa ni juu jamani kama una roho ndogo unaweza ukaanguka kabisa
hapa ni moja na sehemu ya kilele cha ngome hii ya golconda tulivyofika tulikuwa hoi bin taaban,ilibidi tutafute sehemu tukae kupunguza uchovu,hapa nilikuwa nahisi kizunguzungu sana nikaona si vyema kukosa kumbukumbu nyuma yangu ni msikiti wa karne ndani ya ngome hiyoo.karibuni sana hyderabad,karibuni mkajionee wenyewe jinsi ngome ya golconda ilivyokuwa.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!