Rafu za aina hii zinapingwa sana na sheria za mpira wa miguu na ndiyo maana mwamuzi wa mchezo wa jana kati ya Chile dhidi ya Peru, J.Quintana alimtoa nje Ricardo Cruzado (jezi nyeupe) kwa kadi nyekundu. Hiyo ndiyo rafu iliyomvunja Gary medel meno mawili. |
Ulikuwa ni mpepetano wa kutumia nguvu
nyingi sana kati ya timu ya taifa ya Chile dhidi ya timu ya taifa ya
Peru ambapo, mshambuliaji wa Chile na klabu ya Ineter Milan kwa sasa,
Gary Medel amejikuta akipoteza meno yake mawili baada ya kupigwa kiwiko
"kipepsi" na mchezaji wa Peru, Ricardo Cruzado wakati wakigombania mpira
wa juu.
Magoli mawili ya Chile yalifungwa na
mshambuliaji Eduado Vagas kwenye dakika ya 28 na 53, wakati goli la tatu
lilifungwa na Medel dakika ya 34, magoli ambayo yalifanya Chile kutoka
kifua mbele uwanjani baada ya ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Peru.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa dakitari wa timu ya taifa ya Chile,
Giovanni Carcuro, zinasema kwamba, mara baada ya tukio hilo, Medel
alionana na mtaalam wa meno kwa ajili ya kushughulikia jeraha lake, na
muda mfupi atakuwa sawa.
Timu ya taifa ya Peru itabidi ijilaumu
yenyewe kwa uzembe mkubwa waliokuwa nao uwanjani, ambao uliwafanya pia
wakosea penati dakika ya 20 ya mchezo huo.
|
0 comments:
Post a Comment