Searching...
Thursday, October 9, 2014

Cabaye ashoshwa na nafasi nadra PSG

  
Yohan Cabaye




















Kiungo wa Ufaransa na mabingwa wa ligi kuu ya taifa hilo PSG, Yohan Cabaye, amefichua kutamaushwa kwake na nafasi chache anazopewa kuonesha talanta yake kwenye klabu chake.
Mchezaji huyo, 28, ambaye alichezea Lille zamani alirejea Ufaransa na PSG kutoka Newcastle United wa ligi ya Premier ya Uingereza kwa ada ya euro milioni 20 na kusaidia timu hiyo kushinda taji la ligi kuu, Ligue 1 na Kombe la Ligi.
Alidhihirisha umaahiri wake kwenye Kombe la Dunia ambapo Ufaransa walifika robo fainali walipoondolewa kwa unyoya na mabingwa Ujerumani lakini amechezea timu yake Laurent Blanc mara nne pekee musimu huu.
“Bila shaka, nahitaji kucheza. Wakati siko uwanjani, naanza kuhisi mahala pangu pamechukuliwa na mwingine mara moja. Naelewa wakufunzi wana jukumu la kufanya maamuzi na naheshimu hilo na najiambia ni lazima nioneshe ubora wangu zaidi ili kucheza mechi ifuatayo,” Cabaye alisema.
Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps, alimshirikisha kwenye kikosi chake kitakacho wania mechi za kufuzu Kombe la Euro la 2016 na anatumahi kungaria nchi yake kutamshawishi Blanc ampatie muda zaidi kiwanjani.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!