Kazi kwisha: Bosi wa England, Roy Hodgson aliiongoza England kushinda dhidi ya Uswizi
ROY Hodgson amedai timu yake ya England
iliyosheheni vijana wengi imeanza kazi rasmi baada ya Danny Welbeck
kufunga mabao mawili katika ushindi wa jana wa 2-0 dhidi ya Uswizi
kuwania kufuzu Euro 2016.
Mabao hayo yalipunguza presha ya kocha huyo ambaye anakosolewa kwa soka 'mbofu mbofu'.
Ushindi huo wa kwanza katika kampeni za
kufuzu Euro 2016 umekuwa faraja kwa Hodgson ambaye alichemsha vibaya
katika fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini
Brazil.
Alisema: "Hatukuwa na bahati kule Brazil. Kwa sasa tumetoa meno yetu, tutawamaliza na kusonga mbele".
Mkali wa nyavu: Danny Welbeck aliifungia England mabao yote mawili
0 comments:
Post a Comment