IKIWA
kutwaa mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Mfalme, maarufu
kama Copa del Rey haikutosha, Real Madrid pia imeshinda tuzo ya Klabu
Bora ya Mwaka Ulaya.
Sambamba
na mafanikio yao uwanjani, pia wametuzwa kwa programu yao ya kusaidia
jamii, kupitia mradi wa Mfuko wa Real Madrid unaohusu maendeleo na elimu
uliopo mjini El Gallinero.
Mtu wa mataji: Sergio Ramos akibusu taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya Mei mwaa huu
Pedro
López, Makamu wa Rais wa Real, na Emilio Butragueño, Mkurugenzi wa
Mahusiano wa kkabu, walipokea tuzo hizo katika sherehe zilizofanyika
mjini Geneva.
Washindi wengine wa tuzo za ECA mwaka 2014 walikuwa Celtic na Red Bull Salzburg.
Celtic
wameshinda tuzo ya Mafanikio Bora: Tuzo ya Masoko kwa kutumia Uwanja
wao mtandao wa Wi-Fi na simu za mkononi inayorahisisha kuweka taarifa za
mechi, wakati Red Bull Salzburg wamechukua tuzo ya Best Sporting Progress.
Wazee wa tuzo: Real Madrid wameshinda tuzo ya klabu bora ya mwaka Ulaya
0 comments:
Post a Comment