KIKOSI
kipya cha Cameroon kimeendeleza wimbi la ushindi katika kuwania tiketi
za Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Morocco, baada ya jana kuifumua
Ivory Coast mabao 4-1 mjini Yaounde.
Clinton
N'Jie na Vincent Aboubakar kila mmoja alifunga mabao mawili kwa Simba
Wasiofungika huku bao pekee la Tembo wa Ivory Coast likifungwa na
Mwanasoka Bora Afrika, Yaya Toure.
Aibu yao: Yaya Toure aliiongoza Ivory Coast jana ikifungwa 4-1 Cameroon iliyosukwa upya baada ya Kombe la Dunia
Cameroon
iliyosukwa upya baada ya Kombe la Dunia, ilishinda mechi ya kwanza ya
Kundi D mabao 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
Jumamosi iliyopita.
Cameroon,
Algeria, Kongo Brazzaville, Burkina Faso, Cape Verde, Senegal na
Tunisia zimefanikiwa kushinda mfululizo mechi mbili za mwanzoni wakati
Misri ina hali mbaya baada ya kufungwa mfululizo.
Mabingwa
watetezi Nigeria wameendeleza rekodi ya kutofungwa na kuruhusu nyavu
zao kuguswa na Afrika Kusini, baada ya kulazimisha nao sare ya bila
kufungana 0-0 mjini Cape Town.
Super
Eagles walipambana mno kupata sare hiyo ugenini, baada ya kupoteza
mechi ya kwanza nyumbani mbele ya Kongo Jumamosi iliyopita.
Uganda
imeifunga 2-0 Guinea, Algeria imeshinda 1-0 dhidi ya Mali mjini Blida,
Kongo imeifunga Sudan 2-0 mjini Pointe-Noire, Burkina Faso imeichapa
Angola 3-0 mjini Luanda na Cape Verde imewafunga mabingwa wa 2012 Zambia
2-1 mjini Praia.
Senegal
imeshinda 2-0 dhidi ya Botswana mjini Gaborone na Tunisia imewafunga
mabingwa wa kihistoria Misri 1-0 mjini Cairo, wakiwaacha Mafarao bila
pointi katika Kundi G.
0 comments:
Post a Comment