BEKI
mpya wa Manchester United, Marcos Rojo amerejea kutoka kwenye majukumu
ya taifa lake, Argentina kujiandaa kuanza kuichezea klabu yake hiyo mpya
dhidi ya QPR Jumapili.
Rojo
bado hajaichezea klabu yake hiyo mpya licha ya kusajiliwa wiki tatu
zilizopita kutokana na kuchelewa kupata hati ya kufanyia kazi England.
Aliiwakilisha
nchi yake kwenye Kombe la Dunia na akacheza kwa dakika zote 90 katika
mchezo wa kirafiki dhidi ya Ujerumani, Argentina ikilipa kisasi cha
kufungwa kwenye fainali ya Kombe la Dunia.
Amerudi kazini: Rojo akiwasili katika hoteli anayoshi mjini Manchester baada ya kuwa na timu ya taifa ya Argentina
Muargentina
huyo anatarajiwa kuanza kuichezea United Jumapili katika Ligi Kuu ya
England, baada ya suala lake la hati ya kufanyia kazi kupatiwa ufumbuzi.
Ujio
wa beki huyo ni faraja kwa Louis Van Gaal, ambaye timu yake ilionekana
kuwa na tatizo katika safu ya ulinzi, kiasi cha kufanya vibaya kwenye
mechi za mwanzoni.
Safu
ya ulinzi ya Mashetani hao Wekundu imeyumba baada ya kuondoka kwa
mabeki wote wakongwe mwishoni mwa msimu, Patrice Evra, Nemanja Vidic na
Rio Ferdinand.
0 comments:
Post a Comment