Searching...
Tuesday, September 2, 2014

BLIND TAYARI NI SHETANI MWEKUNDU KABISA

KLABU ya Manchester United imemsajili Daley Blind kwa dau la Pauni Milioni 14 katika jitihada za kocha Louis van Gaal kutatua tatizo la safu ya ulinzi Old Trafford.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uholanzi mara moja amwatumia salamu mashabiki wa timu hiyo kwa kusema; "Ni heshima kusajiliwa na United. Siwezi kusubiri kufanya kazi na klabu dunia,". 
Inamaanisha Van Gaal ametumia zaidi ya Pauni Milioni 150 kwa usajili wa kipindi hiki - ambacho ni kiwango kikubwa zaidi kuwahi kutumiwa na klabu hiyo kwa miaka mitano iliyopita, huku Radamel Falcao naye akiwa mbioni kukamilisha uhamisho wa mkopo.

Tabasamu tupu: Manchester United imemsajili Daley Blind kwa Pauni Milioni 14 kutoka Ajax

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!