MABAO
mawili ya Cristiano Ronaldo, moja kila kipindi yametosha kuipa Real
Madrid ushindi wa 2-0 dhidi ya Sevilla, zote za Hispania Uwanja wa
Cardiff City mjini Cardiff na kutwaa Super Cup ya UEFA.
Sifa
zimuendee nyota wa Wales, Gareth Bale aling'ara akicheza kwenye ardhi
ya nyumbani na kutoa mchango mkubwa katika ushimdi huo. Ronaldo alifunga
bao la kwanza dakika ya 30 na la pili dakika ya 49.
Kikosi
cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Carvajal, Pepe, Sergio Ramos, Fabio
Coentrao, Kroos, Rodriguez, Modric, Bale, Benzema, Ronaldo.
Sevilla: Beto, Coke, Pareja, Fazio, Fernando Navarro, Alex Vidal, Krychowiak, Carrico, Vitolo, Suarez, Bacca.

![]() |
| Wafalme wa Ulaya; Wachezaji wa Real Madrid wakifurahia na taji lao la Super Cup ya UEFA leo |

Mambo safi kabisa: Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid Uwanja wa Cardiff City

Magalactico wapya: Kikosi kipya cha kwanza cha Real Madrid kilichotwaa Super Cup



0 comments:
Post a Comment