Searching...
Sunday, August 17, 2014

RASMI: ALBERTO MORENO ATUA LIVERPOOL KWA PAUNDI MILIONI 12

Kijana mpya: Liverpool wametangaza rasmi kumsajili beki wa kushoto wa Hispania Alberton Moreno.

BEKI wa pembeni wa Hispania, Alberto Moreno amesajiliwa na Liverpool kwa dau la paundi milioni 12.
Makubaliano yalifikiwa mapema wiki hii, lakini klabu imetangaza rasmi mwishoni wa wiki hii.
Kinda huyo mwenye miaka 22 anafurahia mafanikio yake ndani ya miaka miwili iliyopita akiwa ametwaa ubingwa wa mataifa ya Ulaya akiwa na timu ya taifa ya Hispania chini ya miaka 21 mwaka 2013 na baadaye aliingia kikosi cha kwanza cha klabu ya Sevilla.
Moreno alishinda ligi ya Europa msimu uliopita akiwa na Sevilla na alitoa machozi baada ya kupigwa mabao 2-0 na Real Madrid katika mechi ya fainali ya  'UEFA Super Cup' siku ya jumanne.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!