Searching...
Sunday, August 17, 2014

JEURI YA MANENO YA JOSE MOURINHO USIPIME...KAULI YAKE NYINGINE KUELEKEA MECHI YA LEO HII HAPA!

No pressure: Jose Mourinho has revealed he is expecting a tough title challenge this season
Hakuna presha: Jose Mourinho ameweka wazi kuwa atakabiliana na ugumu kuwania ubingwa msimu huu.

JOSE Mourinho amedai kuwa kama timu yake itaishia nafasi ya pili atakuwa hajashindwa licha ya kupewa nafasi ya kutwaa ubingwa na ikiwa imetumia paundi milioni 75 mpaka sasa katika soka la usajili.
Mourinho alimuita Arsene Wenger  'Bingwa wa kushindwa' akirejea ukame wa miaka 9 bila kikombe ingawa ulimalizwa mwezi mei mwaka huu baada ya kushinda kombe la FA.
Mreno huyo amewapunguzia presha wachezaji wake kwa kusema: "Hii ni ligi pekee duniani ambayo timu nne, tano au sita zinashindania ubingwa. Moja tu inaweza kushinda. Unaweza kusema nyingine zimeshindwa? sidhani.
Season opener: Portuguese tactician Mourinho has been preparing his side for Chelsea's game at Burnley
Ufunguzi wa msimu: Mwalimu wa kireno, Jose Mourinho anajiandaa na mechi ya ufunguzi wa ligi kuu dhidi ya  Burnley kesho.

"Jambo moja ni kwamba timu moja inafanikiwa na tano zinashindwa. Jambo jingine ni kwamba timu tatu, nne au tano zinaonesha kiwango cha juu, lakini moja inashinda".

Chelsea wataanza msimu huu katika dimba la Turf Moor dhidi ya Burnley kesho jumatatu na Mourinho aliongeza:
"Siwezi kufanya lolote zaidi ya kusema: "Tunajiona washindani wa ubingwa." Kitu pekee ninachoweza kuongeza ni kwamba, kama unamuuliza kila meneja wa ligi kuu, wewe ni mshindani wa ubingwa?, labda wanne, watano au sita wanaweza kujibu, "Ndiyo'
Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich na bodi ya Stamford Bridge inatarajia kuona Mourinho anashindania ubingwa. 
Lakini wanaelewa kuwa ushindani umeongezeka na wamekubali kuwa kushinda kombe ni jambo gumu zaidi ya huko nyuma.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!