Searching...
Monday, July 21, 2014

TETESI ZA USAJILI: MANCHESTER UNITED YAIMARISHA `MAKOMBORA` YA KUMNASA ARTURO VIDAL KUTOKA JUVENTUS

Manchester United to launch new €54m Vidal bid
Imechapishwa Julai 21, 2014, saa 10:30 jioni

MANCHESTER United wiki hii wapo tayari kuanza kuifukuzia saini ya kiungo wa Juventus, Arturo Vidal kwa dau la Euro milioni 54.
Klabu hiyo ya Old Trafford imejiamini kuwa itamnasa nyota huyo wa Chile katika fainali za kombe la dunia na wanaanza harakati zaidi kumuwinda kiungo  huyo mwenye miaka 27.
Louis Van Gaal ambaye alitambulishwa rasmi kuanza kazi jumatano ya wiki iliyopita, ni shabiki mkubwa wa Vidal na aliwahi kujaribu kumsajili alipokuwa anafanya kazi Bayern Munich mwaka 2011 na amethibitisha kumhijtaji tena.
Mholanzi huyo alijaribu kumshawishi Vidal mapema mwezi Julai, licha ya klabu yake kuambiwa kuwa itawagharimu Euro milioni 56 jumlisha Luis Nani.
Juventus wamemsajili Alvaro Morata kutoka Real Madrid na wanapambana kumnasa Roberto Pereyra, wakati huo huo inapendekezwa kuwa Vidal auzwe ili kupata hela.
Vidal ambaye kwasasa anapumzika nchini Chile kufuatia kumalizika kwa fainali za kombe la dunia, hivi karibuni alisema hatima yake Turin ipo mashakani.
“Sidhani kama muda wangu Juventus umekwisha, ingawa siwezi kusema kwasasa,” aliiambia Radio ya Chile. “Nitakaporudi kutoka Chile, nitazungumza na mabosi wangu na tutaona kitakachotokea”.
Mkurugenzi wa Juve, Pavel Nedved alisema klabu inaona ugumu kuwauza Vidal na Pogba, lakini alikiri dau kubwa linaweza kuwalazimisha kufanya biashara.
‘Mipango yetu ipo wazi, tunataka kuwabakisha wachezaji wote muhimu wakiwemo Vidal na Pogba,” . Aliwaambia Tuttospot. “Hatudhani kama tutauza mchezaji yeyote hususani Vidal”.

‘Lakini kama kuna dau kubwa, tunaweza kulifikria hilo, lakini hatutaki kuuza mabingwa wetu”.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!