Searching...
Thursday, July 24, 2014

MASHETANI WEKUNDU WAITUNGUA LA GALAXY 7-0, ONYO KWA MOURINHO, WENGER......


LOUIS Van Gaal ni kiboko. Awaonya Jose Mourinho na Asernal Wenger kuwa amekuja kufanya kazi Old Trafford.
Jana usiku ameshusha majanga kwa LA Galaxy baada ya kuitandika mabao 7-0 katika mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya kabla ya Msimu nchini Marekani.
Hii imezidi sasa! Van Gaal atakuwa anawaomba viongozi wa Manchester United kuipeleka timu kwenye ziara ya maandalizi ya kabla ya msimu kila majira ya kiangazi.
Ikiwa ni siku moja tu imepita tangu alalamike kuhusu ziara ya Marekani kwa madai kuwa inawafanya wachezaji wake wachoke, kocha huyo mpya wa Man United aliitazama timu yake ikipata ushindi mkubwa na kuonesha kiwango kizuri. 
Roo beauty: United forward Rooney is congratulated by Danny Welbeck after his first goal
Raha tupu: Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney  akimpongeza Danny Welbeck baada ya kufunga bao la kwanza.

Mabao ya Man United yalifungwa na Welbeck dakika ya 13, Rooney dakika ya 41 (kwa penati) na dakika ya 45. Mengine yalifungwa na James dakika ya 62, 84 na mawili ya mwisho yalifungwa na Young katika dakika za 88 na 90.

Kikosi cha Man United kipindi cha kwanza (3-4-3): De Gea; Smalling, Jones, Evans; Valencia, Fletcher, Herrera, Shaw; Mata; Welbeck, Rooney. 
Kikosi cha Man United kipindi cha pili (3-4-3)Lindegaard; M Keane, Fletcher, Blackett; Rafael, Cleverley, Herrera, James; Kagawa; Nani, Young. 

Kiosi cha LA Galaxy: Penedo; Gargan, Meyer, Leonardo, DeLaGarza; Ishizaki, Sarvas, Juninho, Husidic; Keane, Zardes.
Alioneshwa kadi ya njano: Keane, Leonardo.
Flying start: Welbeck celebrates putting United in the lead after just 13 minutes
Mwanzo mzuri: Welbeck akishangilia baada ya kuifungia Man United goli la kuongoza katika dakika ya 13
Spot on: Rooney beats Jaime Penedo to double United's advantage from 12 yards out
 Rooney akimfunga kipa Jaime Penedo kwa mkwaju wa penati na kuandikia bao la pili kwa Man United.
Thumbs up: Van Gaal watches the game from the bench alongside his assistant Ryan Giggs
Van Gaal akitazama mechi akiwa kwenye benchi na msaidizi wake Ryan Giggs

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!