Searching...
Thursday, July 24, 2014

MANCHESTER UNITED YAMRUDISHA PAUL SCHOLES OLD TRAFFORD KUFUNDISHA MAKINDA

Watching brief: Paul Scholes (left) was on the touchline on Tuesday as Salford City took on Stalybridge Celtic, the team he co-owns, in pre-season friendly
Paul Scholes (kushoto) alikuwepo katika mechi ya jumanne wakati  Salford City  inacheza dhidi ya Stalybridge Celtic, klabu ambayo ana hisa, ikiwa ni mechi ya maandalizi ya kabla ya msimu.

Imechapishwa Julai 34, 2014, saa 4:00 asubuhi

MANCHESTER United wamemuambia kiungo wake wa zamani Paul Scholes kuwa milango ipo wazi kwake kurudi kufanya kazi ya ukocha Old Trafford.
Scholes alikuwa sehemi ya benchi la Ryan Giggs wakati alipokabidhiwa timu kwa muda mwishoni mwa msimu wa mwaka jana kufuatia kufukuzwa kazi kwa kocha mkuu David Moyes.
Giggs aliingoza Man United katika mechi nne za mwisho za ligi kuu soka nchini England.
Watu walidhani Scholes ameamua kuitosa Man United majira ya kiangazi baada ya kuwakosoa vikali baadhi ya wachezaji wa timu hiyo kwenye fainali za kombe la dunia nchini Brazil.
Scholes aliuliza kama tayari Wayne Roonye amepita miaka yake  28 ya ubora na aliuliza kwanini klabu imemsajili Luke Shaw kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 30.
 Inafahamika kuwa kocha wa sasa wa Man United Louis van Gaal na mkurugenzi mkuu Ed Woodward bado wanaamini  kiungo huyo nyota wa zamani wa England ana kitu cha kuisaida klabu.
Scholes ameambiwa kuwa klabu itafurahi kama watafanya mazungumzo.
Lakini hatapewa kazi katika timu ya kwanza kutokana na Van Gaal kuridhishwa na wasaidizi wake wa sasa.
Helping out: Scholes was part of Ryan Giggs' coaching set-up at the end of last season
 Scholes alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Ryan Giggs mwishoni mwa msimu wa mwaka jana.
Hata hivyo, United wanataka kumpa kazi Scholes ya kufundisha kikosi cha vijana ili asaidiane na kocha wa sasa Nicky Butt.
"Bado tunatambua thamani na ubora wa juu wa Scholes". Chanzo kutoka United kilisema.

"Milango ipo wazi kwake kurudi".

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!