KOCHA Tim Sherwood amefukuzwa Tottenham Hotspur kiasi cha miezi sita tang aanze kazi White Hart Lane.
Sherwood
alirithi mikoba ya Andre Villas-Boas Desemba kwa Mkataba wa miezi 18,
lakini ameshindwa kuingia katika msimu wa pili na klabu hiyo.
Nje: Tim Sherwood amefukuzwa Tottenham baada ya miezi sita

Nje ya mlango: Levy (katikati) ameamua kumtema Sherwood
Tetesi
za kuondolewa kwa Sherwood zilianza mwezi uliopita, na hatimaye
Mwenyekiti Daniel Levy kutafuta mtu mwingine mwafaka zaidi.
Sherwood
ameshinda mechi 14 kati ya 28 akiwa kazini, akitoa safe nne na kufungwa
10, Spurs ikimaliza katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi,
ikizidiwa pointi 10 na Arsenal iliyomaliza nafasi ya nne.
Mwalimu
huyo mwenye umri wa miaka 45 anaweza kupewa ofa mara moja kurejea
kurejea klabu ya Daraja la kwanza, Brighton baada ya Oscar Garcia
kujiuzulu baada ya kufungwa katika mechi ya Nusu Fainali ya mchujo dhidi
ya Derby
0 comments:
Post a Comment