KOCHA
wa Cameroon, Volker Finke amewajumuisha mshambuliaji mkongwe Samuel Eto
na chipukizi Vincent Aboubakar katika kikosi chake cha awali cha
wachezaji 28 kwa ajili ya Kombe la Dunia.
Nchini
Tanzania Eto'o ni maarufu kwa jina la shemeji, baada ya kukutwa na
kashfa ya kutoka na binti wa Dar es Salaam wakati Cameroon imekuja kwa
ajili ya mechi ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka
2010.
Kikosi
cha Finke kimewabeba pia beki wa Tottenham, Benoit Assou-Ekotto, kiungo
wa Barcelona, Alex Song na nyota wa Rennes, Jean Makoun.
Cameroon
ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kufika Robo Fainali za Kombe la Dunia
mwaka 1990 nchini Italia, lakini tang halo imekuwa haifanyi vizuri.
Cameroon ilifungwa mechi zake taut za kundi lake nchini Afrika Kusini
miaka mine iliyopita.
Mshambuliaji
kinda wa miaka 22, Aboubakar amekuwa na msimu mzuri klabu ya Lorient
nchini Ufaransa, wakati Nahodha Eto'o anajiandaa kucheza fainali zake za
nne za Kombe la Dunia.
Kikosi kamili ni makipa:
Charles Itandje (Konyaspor/Uturuki), Ndy Assembe (Guingamp/Ufaransa),
Sammy Ndjock (Fetihespor/Uturuki), Loic Feudjou (Coton Sport), mabeki; Allan
Nyom (Granada/Hispania), Dany Nounkeu (Besiktas/Uturuki), Cedric
Djeugoue (Coton Sport), Aurelien Chedjou (Galatasaray/Uturuki), Nicolas
Nkoulou (Marseille/Ufaransa), Armel Kana-Biyik (Rennes/Ufaransa), Henri
Bedimo (Lyon/Ufaransa), Benoit Assou-Ekotto (QPR/England) na Gaetang
Bong (Olympiakos/Ugiriki).
Viungo;
Eyong Enoh (Antalyaspor/Uturuki), Jean II Makoun (Rennes/Ufaransa),
Joel Matip (Schalke 04/Ujerumani), Stephane Mbia (Sevilla/Hispania),
Landry Nguemo (Bordeaux/Ufaransa), Alexandre Song (Barcelona/Hispania),
Cedric Loe (Osasuna/Hispania) na Edgar Sally (Lens/Ufaransa).
Washambuliaji;
Samuel Eto'o (Chelsea/England), Eric Choupo Moting (Mainz/Ujerumani),
Benjamin Moukandjo (Nancy/Ufaransa), Vincent Aboubakar
(Lorient/Ufaransa), Achille Webo (Fenerbahce/Uturuki), Mohamadou
Idrissou (Kaiserslautern/Ujerumani), Fabrice Olinga
(Zulte-Waregem/Ubelgiji).
Simba Wasiofungika wapo Kundi A pamoja na wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.
0 comments:
Post a Comment