WAGONGA nyundo wa Mbeya, klabu ya
Mbeya City fc imepangwa kundi B katika michuano mipya ya Baraza la
Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ijulikanayo kwa jina la
`CECAFA Nile Basin` inayotarajia kushika kasi kuanzia mei 22 hadi juni 4
mwaka huu nchini Sudan ikijumuisha timu 16.
Katika droo ya michuano hiyo
iliyopangwa leo, Mbeya City imepangwa na timu za AFC Leopards ya Kenya),
El Merreikh Al Fasher ya Sudan na Elman ya Somalia.
Kundi A: El Merreikh ya Sudan, Victoria University ya Uganda, Malakia ya Sudan Kusini na Polisi ya Zanzibar.
Kundi: Al Ahli Shandi ya Sudan, Al Masry ya Misri, Defence ya Ethiopia na Dkhill ya Djibouti.
Kundi D: Hey Al Arab ya Sudan, Arab Contractors ya Misri, Flambeau ya Burundi na Etincelles ya Rwanda.
Kundi D: Hey Al Arab ya Sudan, Arab Contractors ya Misri, Flambeau ya Burundi na Etincelles ya Rwanda.
Mbeya City fc wamepata nafasi ya kushiriki michuano hii baada ya mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc kujiondoa.
Uongozi wa Mberya City kupitia
kwa mwenyekiti wake Mussa Mapunda umesema nafasi hii ni adimu , hivyo
watahakikisha wanajiandaa vizuri ili kuiwakilisha vizuri Tanzania.
Mapunda alisema nguvu waliyokuwa
nayo katika michuano ya ligi kuu ndio wanaipeleka Sudan na tayari
wachezaji waliopo Mbeya wameanza mazoezi , wengine walikuwa nje ya jiji
hilo wakiendelea kuripoti.
Kocha wa Mbeya City fc, Juma
Mwambusi kwa upande wake amefurahishwa na kupata ratiba mapema, hivyo
anaanza kusuka kikosi chake mapema.
Mwambusi aliyeiongoza Mbeya City
fc kushika nafasi ya tatu msimu uliopita anatarajia kuwadhihirishia
watanzania kuwa klabu hiyo si ya kubeza.
Kwa mara ya kwanza, Mbeya City
mwanzoni mwa mwaka huu walishiriki michuano ya kombe la Mapinduzi
inayoshirikisha klabu kutoka nchi za Afrika Mashariki, lakini walitolewa
mapema na waliporudi ligi kuu waliendeleza kasi yao.
Hii itakuwa mara ya pili
kushiriki michuano inayoshirikisha timu za nje ya nchi kama ilivyokuwa
kwa michuano ya Mapinduzi, hivyo wapenzi wa soka nchini Tanzania wana
hamu ya kuiona Mbeya Cuty ikifanya vizuri.
0 comments:
Post a Comment