
Mamia ya wanachama wa Simba
waliamua kumsindikiza Eveva kuchukua fomu na hii inadhihirisha mapenzi
makubwa waliyonayo kwa mwanachama huyu damu wa Simba.
Eveva ameisaidia Simba kwa zaidi ya miaka 20 japokuwa hajawahi kuwa kiongozi wa kuchaguliwa.
Amewahi kuongoza kamati kadhaa za Simba ikiwemo usajili miaka ya 2000 ambapo alifanya kazi nzuri.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi
huo, Damas Ndumbaro alisema kamati yake haitakuwa na huruma kwa yeyote
atakayeenda kinyuma na kanuni.
0 comments:
Post a Comment