WACHEZAJI
Danny Welbeck, Tom Cleverley na Ashley Young wamepigwa faini na kupewa
onyo kali baada ya kujirusha usiku kucha wakiwa na demu saa kadhaa tu
baada ya Manchester United kutolewa katika Robo Fainali ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
Wanasoka
hao wa kimataifa wa England walipigwa picha jijini Manchester usiku wa
Ijumaa iliyopita hadi asubuhibaada ya kurejea kutoka Munich Alhamisi
ambako Jumatano walitolewa na Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa.
Kocha
David Moyes aliwaita watatu hao kuzungumza nao jana makao makuu ya
United, Carrington kabla ya kuwataka wafanye mazoezi ya ziada tofauti na
wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Wachezaji wote watatu wamepigwa faini, ingawa haiko wazi kama wamekatwa mishahara ya wiki mbili au tatu.
Kujirusha kumewaponza: Welbeck kushoto akizungumza na demu waliyekuwa wakicheza naye na kulia ni Cleverley
Moyes,
ambaye atamenyana na klabu yake ya zamani Everton Uwanja wa Goodison
Park Jumapili, ana mpango wa kutumia Pauni Milioni 150 kusajili mwishoni
mwa msimu ili kukijenga upya kikosi chake.
Habari njema kwa Moyes, ni kupata nafuu kwa mshambuliaji Robin van Persie kutoka maumivu yake ya goti.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi ameweka ciedo kwenye Facebook inayomuonyesha akifanya mazoezi peke yake gym.
0 comments:
Post a Comment