Tanzania yatinga Fainali za Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani
Kwa
mara ya pili mfululizo timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani kutoka
Tanzania imetinga fainali za mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto wa
Mitaani baada ya kuchachafya timu ngumu ya Marekani magoli 6 kwa 1,
kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya mashindano haya hapa Rio de
Janeiro.
Tanzania
ilikuwa ya kwanza kupata goli katika dakika ya pili ya mchezo goli
likifungwa na Michael, baada ya kuingia goli hilo Marekani waliweza
kupoteana na kuwafanya vijana wa Tanzania waliokuwa wakitandaza soka
safi kufunga magoli mengine matatu ya haraka haraka na kufanya matokeo
ya mchezo kuwa magoli manne kipindi cha kwanza.
Kipindi
cha pili Tanzania ilizidi kuishambulia marekani na kufanikiwa kufunga
magoli mengine mawili ya haraka haraka na kuifanya Tanzania kufikisha
magoli sita katika mchezo huo wa nusu fainali huku mshambuliaji wa
Tanzania Michael akifunga magoli manne nakuweza kuibuka nyota wa mchezo.
Goli
la Marekani lilifungwa na katika dakika za mwisho za mchezo baada ya
kipa wa Tanzania Emmanuel kuutema mpira mkali uliopigwa kuelekea golini
kwake na baadae mchezajiwa Marekani kuukwamisha wavuni.
Tanzania
leo imetandaza soka safi la kuvutia huku wakipiga mikwaju hatari
kuelekea goilini kwa Marekani, waioonekana kupotea kabisa. Mpaka
wanaingia nusu fainali Marekani walikuwa hawajapoteza mchezo wowote, na
waliweza kuwafunga wenyeji Brazil magoli matani kwa matatu kwenye mchezo
wao wa robo fainali.
Timu
nyingine iliyoingia kwenye fainali ni Burundi baada ya kuifunga
Pakstani magoli 4 kwa matatu, hadi kipindi cha kwanza kinamalizika
Pakistani walikuwa wanaongoza kwa magoli 3 kwa moja, kipindi cha pili
Burundi waliweza kurudisha magoli yote na kuweza kuongoza na kushinda
jumla ya magoli manne kwa matatu.
Hivyo
Tanzania itacheza na Burundi kwenye mchezo wa fainali hapo kesho kwenye
uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense katikati ya Jiji la
Rio de Janeiro huku mgeni rasmi wa mechi hii akiwa Waziri wa fedha wa
Uingereza, George Osborne, Waziri wa jinsia na Watoto na pia Meya wa
Jiji la Rio de Janeiro.
Ikumbukwe
kuwa katika mechi ya kwanza katika kundi 2 la michuano hii Tanzania
ilicheza na Burundi na kutoka sare ya magoli mawili kwa mawili. Huku
Burundi ikirejesha magoli yote mawili katika kipindi cha pili. Mechi ya
fainali kesho itakuwa ngumu sana kwani Burundi wana wachezaji wengi
waliozidi umri, na wanatumia nguvu kubwa sana. Tanzania itawatengemea
wachezajia wake wanaocheza kitimu zaidi na wenye kuweza kupiga mashuti
langini mwa timu pinzani.
Habari na Mutani Yangwe
Mkurugenzi wa TSC Academy (Kutika Rio de Janeiro, Brazil
0 comments:
Post a Comment