Kuwaondoa
wachezaji watatu wakongwe mwishoni mwa msimu (Nemanja Vidic, Rio
Ferdinand na Patrice Evra) inaweza kuleta balaa kwa Manchester United.
Wakati Ferdinand na Vidic wamekuwa wakiandamwa na majeruhi hasa kwa
upande wa Ferdinand, Evra, kwa kutokuwa na majeruhi na consistency
aliyonayo, bado ni chaguo la kwanza katika kikosi cha kwanza. Je ni
kweli beki wa pembeni ambaye ni mzuri sana katika kushambulia na mwenye
uzoefu mkubwa wa kucheza na kuongoza wenzie hana mahala kwa kwenda pindi
anapopoteza kasi kidogo? Lakini kiwango cha Philip Lahm kinaonyesha
hali tofauti.
Evra
na Lahm tunawafananisha vipi? Katika uzuiaji, Evra amefanikiwa kwa
asilimia 50 zaidi katika tackling kuliko Lahm msimu huu, kafanya
interceptions asilimia 30% zaidi ya Lahm. Ingawa Lahm amefanikiwa zaidi
katika upigaji wa pasi, lakini pia Evra ameokoa mara 5 zaidi ya nahodha
wa Bayern, katika kuangalia tofauti yao kulingana na majukumu ya nafasi
wanazocheza. Katika ushambuliaji - Evra amefanikiwa kufanya driblling
zaidi ya Lahm ingawa anazidiwa kwenye key passes.
Ingawa
takwimu hazifanani kutoka na nafasi tofauti wanazocheza, wachezaji wote
wawili walikuwa bora kabisa kwenye nafasi zao wakati walipokuwa kwenye
viwango vyao vya juu kabisa na wote wana uwiano mzuri wa kushambulia na
kuzuia. Wakati Lahm anaweza kuwa katika kupiga pasi, Evra na nguvu zaidi
hewani, na kasi na uwezo kufanya dribbling zaidi.
Je
ni namna gani Evra anaweza kufiti katika kiungo? Katika mfumo wa
4-1-4-1? Hapana, lakini katika mfumo wa 4 2 3 1 kwa pamoja na Michael
Carrick, Darren Fletcher au Maruoane Fellaini. Hahitaji kuwa Paul
Scholes kupiga mipira mirefu kutoka kona moja ya uwanja mpaka nyingine,
au kuwa kama Roy Keane katika ukabaji lakini hatokuwa na ulazima kufanya
tackles dhidi ya mawinga wenye kasi. Kasi yake, ubunifu, stamina,
aggression, uzoefu ni sifa nzuri zinazohitajika kwa kiungo yoyote, Man
Utd wanahitaji sana mtu mwenye sifa hizo.
Kama
tulivyoona usiku wa Jumanne, United wanaweza wasihitaji sana kuangalia
mbali kupata mtu wa kuvaa viatu vya Evra. Katika mechi iliyopewa jina la
utani David vs.Goliath, kiwango cha Buttner’ kilimtuliza Arjen Robben
kwa kiasi fulani, uizingatia uzoefu wake wa mechi kubwa kama zile
Buttner alijitahidi sana. Ingawa mechi moja inaweza isiwe kipimo
(unakumbuka ya Macheda 2009) lakini bado anastahili pongezi kwa jitihada
zake na anastahili kupewa nafasi ili aonyeshe uwezo kama ataweza
kurithi nafasi ya Evra kwa kuwa na consistency.
Kwa
upande mwingine Evra anaweza kuleta ubunifu kwenye kiungo pembeni ya
Fletcher, Carrick auana nguvu hewani, mzuri kwenye tacklin, na uzoefu,
stamina na mzuri katika kuhamasisha timu. Pia kwa upande mwingine United
wanaweza kumuacha Evra aondoke na kuendeleza kujaza listi ya wachezaji
wa kusajili......kumchezesha Evra kati inaweza kuwa plan nzuri, inaweza
pia isikubali kama ilivyokubali kwa Lahm, lakini Moyes hana cha
kupoteza.
0 comments:
Post a Comment