MWANASOKA
bora wa Afrika, Yaya Toure amerejea kwa kishindo na kuiwezesha
Manchester City kurejea kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England
kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji Crystal Palace.
Toure
alimtengenezea nafasi ya kufungta bao la kwanza Edin Dzeko dakika ya
nne ambalo linakuwa bao lake la 24, kabla ya yeye mwenyewe kufunga bao
lake la 23 msimu huu dakika ya 43.
City inabaki nafasi ya tatu sasa ikiwa inazidiwa pointi tatu na vinara Liverpool na pointi moja Cheslea iliyo nafasi ya pili.
Tunatisha: Samir Nasri akishangilia na Edin Dzeko na juu ni Yaya Toure akishangili bao lake
0 comments:
Post a Comment