HATIMAYE
kocha David Moyes amefukuzwa Manchester United baada ya miezi 10 na
sasa Ryan Giggs atakaimu nafasi yake wakati mchakato wa kusaka kocha
mpya ukiendelea.
Mtendaji
Mkuu, Ed Woodward aliwasili Carrington majira ya Saa 2:00 asubuhi leo
kumueleza kocha huyo Mscotland uso kwa uso habari za kufukuzwa kwake.
Moyes aliushukuru uongozi wa klabu baada ya mazoezi juu ya kuondka kwake. Wachezaji hawakuwapo wakati huo.
Taarifa
katika akaunti ya Twitter ya klabu imesema: 'BREAKING: Manchester
United inatangaza kwamba David Moyes ameondoka klabuni. Klabu inapenda
kumshukuru kwa kazi ngumu, ukweli na weledo alioleta kwenye timu.
Ryan Giggs atakuwa kocha wa muda kumalizia msimu.
Iligundulika
jana familia ya Glazer ambao ni wamiliki wa United, ilipoteza imani na
Moyes baada ya timu hiyo kuboronga kwenye Ligi Kuu England na kuangukia
nafasi ya saba kwenye msimamo.
Kipigo
cha mwisho cha mabao 2-0 Jumapili kutoka kwa Everton, ambacho ni cha 11
katika Ligi Kuu msimu huu na kinawafanya mabingwa hao watetezi wazidiwe
pointi 13 kwenye nafasi za ubingwa- ndio kimehitimisha safari yake.
Uthibitisho: Taarifa ya Manchester United kwenye Twitter
Anawasili: Ryan Giggs, ambaye atakuwa kaimu kocha mkuu hadi mwishoni mwa msimu, akiwasili makao makuu ya klabu Carrington leo
Mapema asubuhi ya leo Makamu Mwenyekiti, Ed Woodward alimpelekea taarifa Moyes uso kwa uso juu ya kufukuzwa kwake
DAVID MOYES MAN UNITED
Amecheza mechi 51
Ameshinda mechi 27
Ametoa sare mechi 9
Amefungwa mechi 15
Asilimia ya ushindi ni 52.94
Ameshinda mechi 27
Ametoa sare mechi 9
Amefungwa mechi 15
Asilimia ya ushindi ni 52.94
Kichapo
cha juzi cha mabao 2-0 kutoka kwa Everton ndicho kilihitimisha maisha
ya Moyes United kwa sababu kilimaanisha timu hiyo ilikuwa imepoteza
mechi yake ya 11 msimu huu na wako nyuma kwa pointi 13 kutoka katika
nafasi ya nne.
Familia
ya Glazer na Mtendaji Mkuu wa United, Ed Woodward walikuwa wamepania
kumvumilia Moyes, lakini wameona kiwango cha timu yao kinazidi
kuporomoka kila wiki na wachezaji wanaonekana kuacha kujitoa kwa ajili
ya kocha wao.
Makocha
Jurgen Klopp wa Borussia Dortmund, Louis van Gaal wa Uholanzi na Carlo
Ancelotti wa Real Madrid wanatajwa kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya
kuchukua ukocha wa kudumu mwishoni mwa msimu.
Licha
ya usajili wa fedha nyingi kwa Marouane Fellaini wakati wa kiangazi na
Juan Mata, Januari, United imeshindwa kupambana na wapinzani wao kwenye
mbio za ubingwa.
Moyes
ambaye alirithi mikoba ya Sir Alex Ferguson wakati wa kiangazi, pia
amechemka kwenye michuano mingine msimu huu, United ilitolewa na Swansea
City katika hatua ya tatu ya Kombe la FA, wakati Sunderland waliwatoa
kwenye nusu fainali ya Kombe la Ligi na Bayern Munich kwenye Ligi ya
Mabingwa.
Katika michuano yote Moyes kashinda mechi 27 kati ya 51 akitoka sare mara nane na kufungwa mara 15.
MECHI ZILIZOBAKI
Aprili 26 Norwich City (nyumbani)
Mei 3 Sunderland (nyumbzani)
Mei 6 Hull City (nyumbani)
Mei 11 Southampton (ugenini)
Mei 3 Sunderland (nyumbzani)
Mei 6 Hull City (nyumbani)
Mei 11 Southampton (ugenini)
Katika
hatua nyingine uongozi wa Manchester United chini ya Familia ya Glazer
na Ed Woodward, tayari una majina matatu ya makocha wakubwa ambao
wamekuwa na mafanikio makubwa msimu huu, ambapo jina la kwanza na ambalo
linapigiwa chapuo kubwa ni la Jurgen Klopp ambapo uongozi wa Man
umekubali kulipa fedha kwa ajili ya kuvunja mkataba wake mrefu na
Borussia Dortmund .
Kocha
mwingine Laurant Blanc ambaye amewahi kucheza United na kwa ni kocha
Paris Saint-Germain, -(PSG) mabingwa wapya wa Ufaransa. Hata hivyo
uongozi wa United umekiri kuwepo kwa ugumu wa kumpata Blanc kutokana na
mkataba wake, ingawa wanaamini anaweza kuvutiwa na uzalendo wake kwa
timu hiyo ya Old Trafford.
Diego
Simeone anayetamba hivi sasa na Atletico Madrid, naye yumo katika
orodha hiyo ya kuchukua nafasi ya Moyes, na uongozi huo umesema
hawatakuwa na pingamizi lolote kuvunja benki kwa ajili ya kumpata mtu
sahihi kwa mafanikio ya United.
0 comments:
Post a Comment