Searching...
Monday, April 28, 2014

DANI ALVES ATUPIWA NDIZI NA WABAGUZI WAPUUZI WA HISPANIA, AWAONYESHA JEURI, AOKOTA HALAFU

Dani Alves ametupiwa ndizi zikiwa ni alama sahihi za upuuzi wa watu wenye hisia za kibaguzi nchini Hispania wakati timu yake ya Barcelona ilipokuwa inapambana na Villarreal na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Mashabiki hao walimtupia ndizi Alves raia wa Brazil wakati anakwenda kupiga kona, naye akawaonyesha jeuri.


Alvez ambaye aliwahi kuja jijini Dar es Salaam akiwa na timu ya taifa ya Brazil na kuivaa Taifa Stars katika mechi ya kirafiki, aliikota ile ndizi, haraka akaimenya na kuila.
Baada ya kufanya hivyo, akarudi nyuma tena na kuichonga kona kama alivyokuwa amepanga huku akiwaacha midomo wazi wabaguzi hao.
SAY NO TO RACISM


0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!