Searching...
Thursday, May 23, 2013

MWINYI ATAKA NOVEMBA 30 KUWA MAPUMZIKO AFRIKA MASHARIKI

Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha ripoti ya utafiti juu ya ushirikishwaji wa raia katika mchakato wa uanzishwaji wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika jan a jijini Dar es Salaam. Pamoja nae ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Dira ya Afrika Mashariki (VEAF),  ambao ndio waliofanya utafiti huo,Dr. Azaveli Lwaitama.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (katikati) akizindua kitabu cha ripoti ya utafiti juu ya ushirikishwaji wa raia katika mchakato wa uanzishwaji wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC). Pamoja nae ni Katibu Mkuu wa zamani wa EAC, Balozi Dk. Juma Mwapachu (kulia) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Dira ya Afrika Mashariki (VEAF),  ambao ndio waliofanya utafiti huo,Dr. Azaveli Lwaitama.
 Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (walioketi katikati) akiwa pamoja na washiri wa Kongamano hilo. ******  *******

Na Mtuwa Salira wa EANA
Rais wa zamani wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi amependekeza kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutangaza Novemba 30 kuwa siku ya mapumziko kwa nchi zote za jumuiya hiyo ili kuongeza uelewa wa wananchi wake juu ya masuala ya mtangamano.

Novemba 30, 1993 ilikuwa ndiyo siku ambapo Kamisheni ya Utatu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ilizinduliwa na hatimaye kuzaliwa upya kwa jumuiya hiyo iliyokufa mwaka 1977. Hivi sasa tarehe hiyo inaadhimishwa kama Siku ya EAC lakini siyo siku ya mapumziko katika nchi wananchama.

Mwinyi alitoa mapendekezo hayo Jumatano jijini Dar es Salaam alipozindua ripoti ya  utafiti wa kwanza wa Afrika Mashariki juu ya ushiriki wa raia katika mchakato wa ushirikiano wa EAC, uliyofanywa na Jukwaa la Dira ya Afrika Mashariki (VEAF) ambayo imebaini kwamba upo ushiki hafifu wa raia katika mwenendo mzima wa mchakato huo.

''Nitakuwa na furaha zaidi kutoa mchango wangu wa kuwashawishi marais waliopo sasa ili kutangaza Novemba 30, 1993, siku ambayo Tume ya Utatu ya Afrika Mashariki ilipozinduliwa mjini Arusha, marehemu Mwalimu Nyerere akiwepo, kuwa Siku ya Afrika Mashariki,'' alisema Mwinyi ambaye wakati huo alikuwa Rais wa Tanzania.

Alisema, siku kama hiyo wananchi pamoja na mambo mengine wanaweza kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na maonyesho ya utamaduni na bidhaa za kilimo na viwanda katika majiji yote na mipakani, ambapo alisema, mwisho wa siku vitaongeza uelewa wa wananchi juu ya jumuiya yao ya Afrikia Mashariki. 

Sehemu ya ripoti hiyo ilisema ingawa kuanzsihwa upya kwa jumuiya hiyo kulilenga iwe na misingi yake kwa wananchi, matokeo ya umoja huo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!