Searching...
Wednesday, April 24, 2013

SAKATA LA JUMA NATURE KUTIMULIWA CHANNEL 5 ALIPOINGIA NA NDALA LACHUKUA SURA MPYA ....

Kitendo cha mtangazaji wa EATV Sam Misago kumtoa nje ya studio Sir Juma Nature weekend iliyopita baada ya kwenda studio kwenye kipindi cha Saturday Night Live akiwa na ndala na kaoshi, hajakichukulia poa staa huyo.
Misago 2
Licha ya kuwasilisha malalamiko yake kwenye Facebook kutokana na kitendo hicho, Nature hajaishia hapo na sasa amemchana mtangazaji wa kipindi hicho kwenye wimbo mpya wa TMK HalisiFitina.
Katika wimbo huo Nature anachana, Halafu watu wengine sijui wanakuwaga ni mapimbi, eti msanii kaingia studio na ndala na amevaa pensi hakujua anayosema kwenye Facebook na Twitter sijui kisa hela alizopewa na mameneja feki wasiopenda wa Uswazi, mzomeeni huyo, sasa kazi kwake na raia wake.”

Edited:by Abuu

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!