Searching...
Friday, November 2, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE ZIARANI JIJINI ARUSHA

  Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kuzindua rasmi ujenzi wa barabara za jiji jipya la Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa sherehe za kihistoria za kuuzindua rasmi mji huo wa…
 
Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kuzindua rasmi ujenzi wa barabara za jiji jipya la Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa sherehe za kihistoria za kuuzindua rasmi mji huo wa kitalii kuwa jiji.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionesha ufunguo aliokabidhiwa na Meya wa Jiji la Arusha Mstahiki Gaeudence Lytimo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa sherehe za kihistoria za kuuzindua rasmi mji huo wa kitalii kuwa jiji.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea  ufunguo wa kuwa mkaazi wa heshima wa Arusha toka kwa  Meya wa Jiji la Arusha Mstahiki Gaeudence Lytimo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa sherehe za kihistoria za kuuzindua rasmi mji huo wa kitalii kuwa jiji.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi hati rasmi ya kuuzindua mji wa Arusha kuwa jiji Meya wa Jiji la Arusha Mstahiki Gaeudence Lytimo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mhe Joshua Nassari akiwa ameketi bega kwa bega na Mama Mary Chatanda katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa sherehe za kihistoria za kuuzindua rasmi mji huo wa kitalii kuwa jiji.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea shukrani toka kwa  Meya wa Jiji la Arusha Mstahiki Gaeudence Lyimo baada ya kuzindua nembo ya jiji jipya la Arusha katika Mnara wa Azimio la Arusha jijini humo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua pazia kuzindua rasmi nembo ya jiji la Arusha katika Mnara wa Azimio la Arusha jijini humo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa meza kuu na viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua rasmi nembo ya jiji la Arusha katika Mnara wa Azimio la Arusha jijini humo.



0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!