Searching...
Monday, November 5, 2012

JK AWEKA JIWE LA MSINGI BARABARA YA ARUSHA-MINJINGU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier  wakiweka  jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Arusha Minjingu maeneo ya kijiji cha Mguu-wa-Zuberi wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
Rais Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Arusha baada ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Arusha Minjingu maene ya kijiji cha Mguu-wa-Zuberi wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Frederick Sumaye wakati wa mkutano wa hadhara mjini Katesh mkoani Manyara
Rais Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi wa  mkoa wa Arusha baada ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Arusha Minjingu maene ya kijiji cha Mguu-wa-Zuberi wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier akipanda mti kama kumbukumbu baada  ya  Rais Kikwete kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Arusha Minjingu maene ya kijiji cha Mguu-wa-Zuberi wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
Sehemu ya barabara ya Minjingu-Babati-Singida iliyozinduliwa na Rais Kikwete
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Tonia Kandiero wakifurahia baada ya kuzindua barabara ya Minjingu-Babati-Singida nje kidogo ya mji wa Babati Mkoa wa Manyara. Anayeshuhudia kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John  Pombe Magufuli na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji) Dkt Mary Nagu
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Tonia Kandiero na viongozi wengine wakikata utepe  kuzindua barabara ya Minjingu-Babati-Singida nje kidogo ya mji wa Babati Mkoa wa Manyara. Anayeshuhudia kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John  Pombe Magufuli na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji) Dkt Mary Nagu
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mhe Rose Kamili baada ya kuzindua mradi mkubwa  wa maji  wa Mwakonko Singida Mjini.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!