Searching...
Monday, June 25, 2012

Italia yafuzu kuingia nusu fainali


England na Italia
Timu zote mbili zilishindwa kuzitumia nafasi zilizojitokeza katika muda wa dakika 120 kufungana mabao
Timu ya England ya soka imeondolewa katika mashindano ya Euro 2012, baada ya kufungwa na Italia usiku wa Jumapili katika robo fainali, kwa kufungwa magoli 4-2 ya penalti mjini Kiev, Ukraine, kufuatia muda wa kawaida na dakika 30 zaidi kumalizika kwa timu hizo mbili kutofungana.
Italia sasa itapambana na Ujerumani katika mechi ya nusu fainali.
Alessandro Diamanti alifunga bao la kuamua mshindi katika mikwaju hiyo ya penalti, baada ya Ashley Young na Ashley Cole kukosa kufunga mabao kupitia mikwaju waliyopiga.
Vijana wa meneja Roy Hodgson ilikuwa wazi walilemewa katika mchezo mzima, lakini ni hali ya imani na uvumilivu iliwafanya kuwa na matazamio ya kuishinda Italia.
Italia iliweza kugonga mwamba, na bao la Antonio Nocerino lilikataliwa baada ya mwamuzi kusema aliotea mpira.
Kadri mechi ilivyoendelea, ndivyo wachezaji wa England nao walionekana wachovu, na ikielekea walitazamia bahati zaidi kuliko kujitahidi kuimarisha kiwango cha mchezo wao, na penalti kwao bila shaka ikawa sio za kutegemewa tena.
Baada ya mechi, nahodha Steven Gerrard alisema: "Wachezaji walicheza kadri ya uwezo wao wote. Nilidhani tungelipata bahati katika mikwaju ya penalti, lakini mambo hayakuwa hivyo. Ukiongoza katika penalti, unashikilia matumaini kwamba mambo yatasalia hivyo, lakini Italia ndio waliokuwa na bahati. Vijana waliokuwa walinzi walifanya kazi nzuri mno, na kuiletea nchi fahari, lakini tunarudi nyumbani na mioyo ya huzuni, na hili ni jambo gumu kulikubali."

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!