
Fuvu za vichwa vya Wanyarwanda waliouawa mwaka wa 1994
Mahakama ya uhalifu wa kivita kwa ajili ya Rwanda imemhukumu kifungo
cha maisha jela afisa wa zamani wa Rwanda Callixte Nzabonimana kwa
mauaji ya halaiki. Mahakama hiyo ya kimataifa kwa ajli ya Rwanda
ilisema waziri huyo wa zamani alichochea mauaji ya watu kati ya 15 hadi
60 wa kabila la Tutsi mwezi Aprili mwaka wa 1994 katika eneo la
Nyabikenke. Ilisema pia kuwa alichochea watu mara tatu hadharani mwezi
huo kuwauwa Watutsi na akaingia kwenye makubaliano ya kuwauawa watu wa
kabila hilo na serikali ya muda ya Rwanda wakati huo. Nzabonimana
alikuwa waziri wa maswala ya vijana wa Rwanda katika serikali ya muda
iliyoundwa mwaka wa 1994. Alikamatwa mwezi Februari nchini Tanzania na
kukabidhiwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa ajili ya Rwanda yenye
makao yake mjini Arusha, Tanzania. Wanamgambo wa Kihutu inakisiwa
waliuawa watu laki 8 wa kabila la Tutsi na Wahutu wenye msimamo wa kadri
wakati wa mauaji ya halaiki mwaka huo wa 1994. Mahakama hiyo
inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ilibuniwa kwa ajili ya kusikiliza
kesi dhidi ya wahusika wakuu wa mauaji ya halaiki ya Rwanda.
0 comments:
Post a Comment