Searching...
Monday, December 5, 2011

Waziri wa Maji,Profesa Mark Mwandosya Alipozungumza na Waandishi wa Habari Ofisini Kwake Siku Chache baada ya Kurejea Kutoka Nchini India Kwa Matibabu

Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya (kulia ) akizungumza na viongozi watendaji wakuu wa wizara hiyo na waandishi wa habari kuhusu kutoa shukurani kwa watu mbalimbali waliokuwa wakimjulia afya yake na kumwombea, akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal ,Waziri Mkuu,Mizengo Pinda, Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, viongozi wa dini na wa kisiasa ambao ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad , na Profesa Ibrahim Lipumba na wananchi Watanzania kwa ujumla bila kujali Itikadi za kisiasa.Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Gerson Lwenge .
Waziri wa Maji,Profesa Mark Mwandosya wa pili kutoka (kushoto)akiwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Mhandisi Christopher Sayi wa pili kutoka (kulia) wakati akielekea katika ukumbi wa mikutano wizarani hapo kwa ajili ya kuzungumza na baadhi ya watendaji wakuu wa wizara na waandishi wa habari ili kutoa shukrani kwa watu mbalimbali waliokuwa wakimjulia afya yake na kumwombea. Na wa kwanza kutoka (kulia)ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bashir Mrindoko. Kushoto ni mtoto wa waziri, Emmanuel Mwadosya.
Picha na Richard Mwaikenda

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!