Searching...
Monday, December 5, 2011

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Na Mbunge Wa Kitope Zanzibar Atembelea Jimbo Lake

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Akikabidhi Hati Ya Usajili Wa Saccos Ya Uwezeshaji Kwa Katibu Mkuu Wa Wizara Ya Kazi Bibi Asha Abdulla
 Mbunge Wa Jimbo La Kitope Balozi Seif Ali Iddi Akipokea Msaada Wa Seti Tatu Za Kompyuta Kutoka Kwa Rais Wa Jumuiya Ya Khoja Shia Ithna-Asheri Zanzibar Nd. Mohd Raza.Kompyuta Hizo Zenye Thamani Ya Shilingi Milioni 8,000,000/- Ni Ahadi Iliyotolewa Na Rais Wa Shirikisho La Jumuiya Ya Kimataifa Ya Khoja Shia Ithna-Sheri Dr. Ali Dinna Aliyoitoa Tarehe 30 Mei Mwaka Huu Wakati Wakitoa Msaada Wa Madeski Kwa Skuli Za Jimbo La Kitope.
Mbunge Wa Jimbo La Kitope Balozi Seif Ali Iddi Akikabidhi Seti Za Jezi Na Mipira 46 Kwa Timu 23 Za Soka Zilizomo Ndani Ya Jimbo La Kitope. Vifaa Hivyo Vya Michezo Hutolewa Na Mbunge Huyo Kila Mwaka Ili Kuimarisha Michezo Jimboni Humo.
Mke Wa Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi Akiwanasihi Wake Wa Waheshimiwa Kuwasaidia Waume Zao Majimbo. Mama Asha Alisema Hayo Katika Hafla Fupi Ya Uzinduzi Wa Kikundi Cha Ushirika Cha Hatubaguani Wote Ni Sawa Cha Jimbo La Kitope.
Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Akizindua Kikundi Cha Ushirika Wa Ushoni Cha  Hatubaguani Wote Ni Wetu Cha Jimbo La Kitope. Kikundi Hicho Pia Kimepatiwa Msaada Wa Vyarahani 16 Pamoja Na Baadhi Ya Vifaa Kwa Ajili Ya Kuendeleza Mafunzo Yao Ya Ushoni.
Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Akipokea Maandamano Ya Vikundi Vya Ushirika Vya Saccos Katika Maadhimisho Ya Wiki Ya Uwezeshaji Zanzibar. Sherehe Hizo Zimefanyika Makao Makuu Ya Wizara Ya Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Na Ushirika.
Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Akiwa Katika Picha Ya Pamoja Na Viongozi Wa Wizara Ya Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Na Ushirika Na Baadhi Ya Viongozi Wa Saccos Ya Uwezeshaji.Picha Zote na Ofisi ya Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar
--
Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi amelipongeza Shirikisho la Kimataifa la Jumuiya ya khoja Shia ithna-asheri kwa juhudi zake za kusaidia Maendeleo ya Elimu Hapa Zanzibar.

Balozi Seif alitoa pongezi hizo baada ya Kukabidhiwa Seti tatu za Kompyuta kutoka kwa Rais wa Shirikisho hilo Duniani Dr. Ali Dinna.

Rais wa Jumuiya ya Koha Shia Ithna-sheri hapa Zanzibar Nd. Mohd Raza amekabidhi msaada huo kwa Niaba ya Rais wa Shirikisho hilo hafla iliyofanyika katika Skuli ya Kitope.

Balozi Seif ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Maendeleo makubwa yamepatikana ndani ya Jimbo la Kitope kutokana na kupata nguvu za Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-sheri.

Aliwaomba wananchi wa Majimbo mengine kuhakikisha wanachagua Viongozi wazuri watakaowaleteta maendeleo ya haraka katika Majimbo yao bila ya kuangalia ujomba au rafiki.

Mapema Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-sheri Zanzibar Nd. Mohd Raza alisema Taasisi yao itaendelea kusaidia huduma za Kijamii, Elimu na Uchumi ili kuona ukali wa maisha unapungua miongoni mwa Wananchi.

Kompyuta hizo zenye thamani ya shilingi milioni nane ni utekelezaji wa ahadi ya Uongizi wa Shirikisho hilo waliyoitowa tarehe 30 Mei mwaka huu wakati wakikabidhi msaada wa madeski katika skuli zilizomo ndani ya Jimbo la Kitope.

Wakati huo huo Balozi seif alizindua Kikundi cha Ushirika cha Ushonaji kiitwacho hatubaguani wote ni wetu cha jimbo la Kitope kinachoendelea kupata mafunzo katika ofisi ya jimbo hilo hapo kinduni.

Balozi Seif pia alikabidhi msaada wa vyarahani, mota pamoja na Vifaa mbali mbali vya kujifundishia vikiwa na thamani ya jumla ya shilingi Milioni 2,325,000/-.

Akitoa nasaha zake katika Hafla hiyo Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi amewaomba Wake wa waheshimiwa kuwasaidia Waume zao katika kufanya ziara za kujua matatizo yanayowakabili Wananchi.

Mama Asha Alisema utaratibu huo utasaidia kuibua matatizo ya msingi na kuleta upendo katika kuharakisha maendeleo ya pamoja kati ya Viongozi na wanaowaongoza.

Kikundi cha ushirika cha ushoni cha hatubaguani wote ni wetu chenye wanachama 45 kimelenga kutoa mafunzo kwa wnanchi wake kwa nia ya kusambaza ajira miongoni mwa wanawake ambao ndio walezi wa
Familia popote pale.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
4/12/2011.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!