Searching...
Tuesday, July 26, 2011

Watu 38 wafariki katika ajali ya reli nchini China


Idara ya reli ya Shanghai imesema, sehemu ya reli ya mji wa Wenzhou mkoani Zhejiang China iliyotokea ajali tarehe 23 kimsingi inafanya kazi tena, na uendeshaji wa reli kutoka mji wa Hangzhou hadi mji wa Shenzhen unarejeshwa hatua kwa hatua.
Habari kutoka serikali ya Wenzhou zinasema hadi saa saba mchana wa tarehe 25, ajali ya reli imesababisha vifo vya watu 38, na wengine 200 kujeruhiwa. Hivi sasa watu waliojeruhiwa wanatibiwa katika hospitali zaidi ya kumi mjini humo. Wataalamu 13 kutoka Beijing, Shanghai na Nanjing wamefika Wenzhou tarehe 24 kushiriki kwenye kazi ya kuwatibu majeruhi.
Baada ya ajali hiyo, rais Hu Jintao wa China na waziri mkuu Wen Jiabao walitoa maagizo mara moja, wakizitaka idara husika zifanye uokoaji kwanza, kuchunguza chanzo cha ajali, na kushughulikia vizuri kazi za baadaye.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!