Searching...
Saturday, July 2, 2011

Uganda na Tanzania kuimarisha miundo mbinu yao

 Mradi wa pamoja wa kuimarisha miundombinu itakayounganisha Uganda na Tanzania unatarajiwa kugharimu dola bilioni 3. Taarifa ya Wizara ya Usafirishaji ya Tanzania imesema mradi huo utakuwa wa aina yake na kwamba utazikurubisha zaidi nchi hizo mbili wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Imeelezwa kuwa kati ya hizo dola bilioni 3, dola bilioni 1.9 zitatumika katika kuunda na kuimarisha mtandao wa reli wa nchi hizo mbili huku fedha zilizosalia zikitumika kuimarisha bandari hususan nchini Tanzania.
Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania Omari Nundu na mwenzake wa Uganda Abraham Byandala walitiliana saini makubaliano ya ushirikiano katikati ya wiki hii na utekelezwaji wake unatarajiwa kuanza mara moja.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!