Searching...
Monday, June 13, 2011

Man U yamsajili Phil Jones

Manchester United imemchukua mlinzi wa Blackburn Rovers, Phil Jones, katika mkataba wa miaka mitano unaoaminika kuwa wa thamani ya pauni milioni 17.
Phil Jones
Ametia saini mkataba wa miaka mitano na Man United
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya England ya vijana chini ya umri wa miaka 21 alikuwa amekaguliwa afya na Manchester United tarehe 8 mwezi huu wa Juni.
Licha ya Arsenal na Liverpool kutaka kumsajili kijana huyo mwenye umri wa miaka 19, hatimaye ameamua kuchezea uwanja wa Man U wa Old Trafford.
"Hii ni nafasi nadra kujitokeza maishani nami natafuta changamoto mpya", alieleza Jones kupitia wavuti ya kijamii ya Twitter.
"Ningelipenda tu kuongeza kwamba nilifurahi sana kuichezea Blackburn na siku zote nitakuwa shabiki mkubwa," alielezea.
Taarifa ya United ilielezea klabu "kilifurahishwa" na hatua hiyo ya kumsajili mchezaji huyo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!