Searching...
Monday, June 20, 2011

Kongamano la umma na Afrika kuhusu sekta utumishi wa umma laanza Dar es salaam Tanzania

Kongamano la sekta ya umma
Kongamano la siku tatu la Umoja wa Mataifa na Afrika linalohusu utumishi wa Umma limeanza leo jijini Dar es Salaam ambako wajumbe zaidi ya 300 kutoka mataifa 80 wanajadilia mbinu mbalimbali za kuboresha utumishi wa umma.
Kongamano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya kwanza barani afrika na nchini Tanzania limeweka shabaa ya kujadili kwa kina ni kwa kiasi gani utumishi wa umma unavyoweza kuharakisha kuleta maendeleo kwa wananchi.
Utumishi wa umma unachukua nafasi kubwa kwenye harakati za ustawi wa jamii na barani Afrika inatajwa kwamba utumushi wa umma unatoa sehemu kubwa ya ajira inayofikia zaidi ya asilimia 70. Kwa kuzingatia hilo wajumbe kwenye kongamano hilo wanania ya kuhakikisha kwamba mfumo na muundo wa utendaji kazi kwenye utumishi wa umma ni ule unaowajibika na ambao unazingatia mageuzi ya uongozi ili kuzaa matunda ya mafanikio kwa wananchi.
Suala la umaskini linalowakabili wananchi wengi hasa katika nchi za dunia ya tatu, ni mada ambayo inatazamiwa kujitokeza zaidi kwenye kongamano hil.
Takwimu za hivi karibuni zinasema kuwa watu zaidi ya bilioni 1 na laki 7 ambao wanatoka katika mataifa 104 yaliyoorodheshwa kuwa mataifa maskini, wanaishi katika hali ya kukatisha tama kutokana na hali ngumu ya maisha wanayokumbana nayo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!