Searching...
Friday, May 20, 2011

Mkutano wa kwanza kuhusu biashara na uwekezaji wafanyika Hangzhou

Gazeti la Renminribao limeripoti kuwa, mkutano wa kwanza kuhusu biashara na uwekezaji kwenye Baraza la utafiti kuhusu mambo ya Afrika umefanyika huko Hangzhou, China.
Mkutano huo unalenga kuhimiza eneo la ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika kuvutia uwekezaji, na kuhimiza viwanda vya mkoa wa Zhejiang na sehemu nyingine nchini China kuanzisha shughuli zao barani Afrika. Pia watu wanaoshiriki kwenye mkutano huo watabadilishana mawazo kuhusu hali ya Afrika na mazingira ya uwekezaji.
Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa suala la Afrika ya China Bw. Wei Jianguo, naibu mkuu wa mkoa wa Zhejiang Bw. Gong Zheng pamoja na mabalozi zaidi ya 160 kutoka umoja wa nchi za kiarabu, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Guinea, Rwanda na Uganda walihudhuria kwenye mkutano huo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!