Searching...
Wednesday, April 13, 2011

United Yaichapa Chelsea 2-1

Magoli mawili ya Chicharito na Ji Sung Park yamein'goa Chelsea katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya.
Chelsea ilienda Old Trafford ikiwa imefungwa bao 1-0, katika mchezo wa kwanza uliochezwa Stamford Bridge na kutakiwa kufunga japo magoli mawili ili isonge mbele.
Gumzo kuu kwa upande wa Chelsea lilikuwa kuanza au kutoanza kwa Fernando Torres, ambaye hajafunga goli hata moja tangu ahamie Stamford Bridge kutoka Liverpool kwa uhamisho wa Pauni milioni 50.
Carlo Ancellotti aliamua kuanza na Torres.
Bao la kwanza la United lilifungwa na Havier Hernandez katika dakika ya 43 ya kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Chelsea walifanya mabadiliko kwa kumtoa Torres na kumuingiza Didier Drogba, ambaye katika dakika ya 77 alitikisa nyavu za Man United.
Hata hivyo bao hilo halikudumu kwa sekunde nyingi kwani Ji Sung Park alipachika bao la pili katika dakika hiyo hiyo.
United sasa wanasonga mbele kucheza nusu fainali, na huenda wakakutana na Schalke 02 au Inter Milan.
Katika mchezo mwingie wa robo fainali, Barcelona wamesonga mbele baada ya kuichapa Shaktar Donetsk 1-0.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!