Searching...
Tuesday, April 12, 2011

Mwanasiasa wa Uingereza achoma moto Qur'ani Tukufu

 Sion Owens mwanachama wa chama cha BNP nchini Uingereza amechoma moto Qur'ani Tukufu kwa lengo la kuvutia uungaji mkono wa wanachama na wafuasi wa chama hicho wampigie kura katika uachauzi wa bunge la Welsh ambao umepangwa kufanyika mwezi ujao. Kwa mujibu wa gazeti la Pakistan la Times Pakistan, mbunge huyo ambaye alionyesha filamu yake mwenyewe akiwa anachoma moto Qur'ani Tukufu hatimaye alitiwa nguvuni na askari wa Uingereza. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza imelaani kitendo hicho ambacho imesema kinakwenda kinyume na thamani za kimaadili. Imesema kuwa serikali ya nchi hiyo haitaruhusu vitendo vya mifarakano na chuki kuenea nchini humo na kwamba watu wote wanapasa kuishi katika mazingira ya utulivu na amani. Mkuu wa idara ya polisi ya Wale Kusini amesema kuwa kitendo hicho cha kukosea heshima matukufu ya kidini hakikubaliki kabisa katika jamii ya Uingereza na kuongeza kuwa wahalifu watapewa adhabu kali. Kukosea heshima matukufu ya Kiislamu limegeuka na kuwa jambo la kawaida kabisa kwa wanasiasa wa nchi za Magharibi wanaotaka kupigiwa kura katika chaguzi mbalimbali.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!