Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linatiwa hofu  na hali ya usalama wa chakula nchini Libya ambako kwa zaidi ya mwezi  mmoja sasa machafuko yamekuwa yakiendelea kwenye miji mbalimbali ikiwemo  Tripoli, Misrata na Benghazi.  
Shirika hilo limesema jinsi vita vinavyoendelea kwa muda mrefu idadi ya watu wanaohitaji msaada wa chakula pia inaongezeka. Libya ni muagizaji mkubwa wa chakula kutoka nje na machafuko yamefanya kuwa vigumu kuingiza chakula cha kutosha.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini  Geneva hii leo kuhusu hali ya usalama wa chakula nchini Libya mkuu wa  WFP kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini Daly Belgasan  amesema nchi hiyo imebakia na akiba ndogo ya chakula cha kutosheleza  muda usiozidi miezi miwili na endapo hatua madhubuti hazitachukuliwa  kuongeza akiba ya chakula basi kutakuwa na matatizo makubwa.
WFP pia imesema inahofia upatikanaji wa chakula kwa maelfu ya watu  waliokwama kwenye maeneo yenye mapigano makali, wakimbizi wa ndani,  wahamiaji na makundi ya watu wasiojiweza.Shirika hilo limesema jinsi vita vinavyoendelea kwa muda mrefu idadi ya watu wanaohitaji msaada wa chakula pia inaongezeka. Libya ni muagizaji mkubwa wa chakula kutoka nje na machafuko yamefanya kuwa vigumu kuingiza chakula cha kutosha.



 
 
0 comments:
Post a Comment