Searching...
Friday, April 29, 2011

Iran yatoa msaada wa zaidi ya dola milioni moja, kusaidia miradi ya kilimo Tanzania

 Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa msaada wa dola milioni moja na laki mbili kwa serikali ya Tanzania, kwa minajili ya kuisaidia nchi hiyo katika kampeni yake ya 'Kilimo Kwanza' inayoanza kushika kasi nchini humo. Taarifa zinasema kuwa, msaada huo ulikabidhiwa na Bwana Bahman Ahmadi Balozi Mdogo wa Iran nchini Tanzania kwa Bwana Lazaro Nyalandu Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania mjini Dar es Salaam. Bahman Ahmadi ameeleza kuwa, msaada huo umetolewa na taifa la Iran kwa shabaha ya kuimarisha uhusiano mwema uliopo kati ya nchi hizo mbili. Ameongeza kuwa, msaada huo utaweza kuisaidia Tanzania katika kukabiliana na upungufu wa chakula pamoja na kuwasadia wakulima kupata mapato mengi. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania ameishukuru serikali ya Iran kwa msaada huo na kuahidi kwamba utatumika kama ilivyokusudiwa. Aidha Nyalandu amewakaribisha wawekezaji kutoka Iran kuja nchini Tanzania na kushirikiana na wazalendo katika kutumia vyema fursa mbalimbali zilizopo hasa katika sekta ya kilimo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!