Searching...
Tuesday, March 22, 2011

Mugabe: Kilichowapeleka Wamagharibi Libya ni mafuta ya nchi hiyo


Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amezilaani vikali nchi za Magharibi akisema kwamba lengo la mashambulizi ya nchi hizo huko Libya si kuwasaidia wananchi bali ni tamaa yao juu ya utajiri wa mafuta wa taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.
Mugabe amezilaumu nchi za Magharibi kwa kutumia vibaya azimio la Umoja wa Mataifa la kuanzisha eneo lililopigwa marufuku kuruka ndege nchini Libya.
Aidha ameulaumu Umoja wa Mataifa akisema kuwa haukupaswa kupasisha azimio hilo ambalo limepelekea wafyonza damu wa Kimagharibi kupata kisingizio cha kuwashambulia watu wa Afrika.
Vile vile amezishambulia nchi za Magharibi kwa kutojali damu za Waafrika akisema kwamba nchi hizo zimekiuka azimio la Umoja wa Mataifa ambalo lengo la kupitishwa kwake lilikuwa ni kumzuia tu kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi asiwashambulie wananchi.
Amesema, yeye na viongozi wengine wa Afrika walikuwa hawakubaliani na muundo wa utawala nchini Libya na walitaka kufanyike mabadiliko, lakini si kwa njia hii ya uvamizi wa nchi za Magharibi ambao wanafanya mashambulizi ya kiholela na kuuwa raia wa Libya wasio na hatia kwa lengo kuhodhi visima vya mafuta vya nchi hiyo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!