Redio ya taifa ya Zimbabwe imemtuhumu Waziri Mkuu wa nchi hiyo Morgan Tsvangirai kwamba anajaribu kuanzisha wimbi la maandamano ya upinzani kama yale yanayoshuhudiwa nchini Misri. Redio hiyo inayodhibitiwa na wafuasi wa Rais Robert Mugabe imetangaza kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Tsvangirai ana nia ya kuwachochea wafuasi wake ili waanzishe mapambano dhidi ya kiongozi wa nchi hiyo anayeongoza Zimbabwe kwa kipindi cha miaka 30 sasa. Redio hiyo imeashiria matamshi ya hivi karibuni ya Morgan Tsvangirai ambaye ameunga mkono mapinduzi ya watu wa Misri na Tunisia na kusema kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja kwamba anaunga mkono hatua kama hiyo nchini Zimbabwe. Msemaji wa Waziri Mkuu wa Zimbabwe Luke Tamborinyoka amesema madai hayo ni upuuzi mtupu.
Wafuasi kadhaa wa Morgan Tsvangirai wamepigwa na kujeruhiwa vibaya katika machafuko ya kisiasa yaliyotokea wiki hii nchini Zimbabwe.


0 comments:
Post a Comment