Maelfu ya wananchi wa Misri bado wametapakaa katika eneo la wazi la Tahrir mjini Cairo, siku moja baada ya kujiuzulu kwa Rais Hosni Mubarak.

Waandamanaji wamekesha Tahrir
Baada ya miaka 30 madarakani, Bw Mubarak alilazimishwa kuondoka madarakani kufuatia siku 18 za maandamano ya kupinga serikali.

Sherehe baada ya Mubaraka kutangaza kuondoka
Rais wa Marekani Barak Obama ameita nchi ya Misri kuwa yenye kuhamasisha, lakini amesema lazima nchi hiyo ielekee katika utawala wa kiraia na wa kidemokrasia.
Rais huyo amemtuma Adm Mike Mullen, mwenyekiti wa wakuu wa jeshi la Marekani, kwenda Jordan na Israel kujadili hali ya mabadiliko ya Misri.

Waandamanaji Tahrir
Mandamano ya kupinga serikali yaliyoanza Januari 25, yalichochewa na kuenea kwa hali ya mashaka nchini Misri, kutokana na ukosefu wa ajira, umasikini na ufisa


0 comments:
Post a Comment