Searching...
Monday, February 7, 2011

Bush afuta safari yake Uswisi kwa kuhofia kutiwa nguvuni kwa kutesa wanadamu

 Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush amefuta safari yake nchini Uswisi akihofia kutiwa nguvuni baada ya jumuiya za kutetea haki za binadamu na kupinga mateso kutoa wito wa kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi ya mwanasiasa huyo anayelaumiwa kwa kuruhusu mateso na kukiuka haki za binadamu. Bush alitazamiwa kuhutubia mkutano wa Wayahudi mjini Geneva lakini mashinikizo ya jumuiya za kimataifa za kutetea haki za binadamu yanayoitaka serikali ya Uswisi imtie nguvuni kwa makosa ya kutesa binadamu na kumfungulia mashtaka ya jinai, yamemlazimisha kukatiza safari hiyo.
Vyombo vya sheria vya Uswisi vimetangaza kuwa mashtaka kadhaa dhidi ya rais huyo wa zamani wa Marekani yamewasilishwa katika mahakama za Geneva. Makundi ya kutetea haki za binadamu yameahidi kuwasilisha mashtaka mengine yanayohusiana na ukiukwaji wa haki za wafungwa wa kigeni katika jela mbaya za Guantanamo Bay na katika korokoro za Marekani huko Iraq, Afghanistan na maeneo mengine duniani.
Bush alikiri katika uzinduzi wa kitabu cha kumbukumbu zake alichokipa jina la Decision Points kwamba aliruhusu mateso dhidi ya washukiwa wa ugaidi.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!